1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yapuuzia mpango wa kumaliza vita kati yake na Urusi

3 Juni 2023

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksii Reznikov amepuuzilia mbali mpango uliopendekezwa na mwenzake wa Indonesia, wa kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine akilitaja pendekezo hilo kuwa la ajabu.

Ukraine Oleksij Resnikow
Picha: Genya Savilov/AFP/Getty Images

Mpango huo ulijumuisha kusitishwa mara moja kwa uhasama , mapigano na wanajeshi kuondoka katika maeneo wanayoyazunguka na maeneo hayo kushikiliwa na vikosi vya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa. 

Pia Waziri wa Ulinzi wa Indonesia Prabowo Subianto alipendekeza kufanyika kwa kura ya maoni itakayosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika maeneo yaliyo na utata.

Subianto alipendekeza hilo katika mkutano wa kilele wa masuala ya usalama unaofahamika kama jukwaa la Shangri-La nchini Singapore. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW