1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yaripoti mashambulizi mapya mjini Kiev

9 Machi 2023

Miji kadhaa nchini Ukraine imeripoti msururu mpya wa mashambulizi ya makombora ya vikosi vya Urusi. Ripoti za mashuhuda zilizosambaa katika mitandao ya kijamii, zimezungumzia milipuko ya hatari mjini Kiev.

Ukraine Krieg | Russische Raketen in Charkiw
Picha: Vadim Belikov/AP Photo/picture alliance

Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegram, meya wa Kiev Vitali Klitschko, amethibitisha kuwa wilaya ya Kusini mwa Kiev, Holosiiv ililengwa na kuongeza kuwa karibu asilimia 15 ya makazi mjini humo kwasasa hayana umeme.

Wagner lasema jeshi la Urusi limezinyakua wilaya kadhaa Ukraine

Mashambulizi ya makombora ya Urusi yanayolenga miundo mbinu ya nishati, pia yamesababisha ukosefu wa umeme katika eneo la Kusini la Odessa nchini humo pamoja na Kharkiv, katika eneo la Mashariki, kwa mujibu wa maafisa katika maeneo hayo.

Kupitia mtandao wa Telegram, gavana wa kijeshi wa Odessa Maksym Marchenko, amesema kutokana na mashambulizi hayo makubwa, kituo kimoja cha nishati cha kikanda kililengwa na jumba la makazi kuharibiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW