1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yasema bado yaudhibiti mji wa Bakhmut

23 Mei 2023

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Hanna Maliar amesema kuwa vikosi vya nchi hiyo bado vinadhibiti ukingo wa kusini magharibi mwa mji wa Bakhmut na kwamba mapigano katika mji huo yamepungua.

Kämpfe und Zerstörung in Bachmut, Ukraine
Picha: LIBKOS /AP/picture alliance

Bi Maliar ameandika katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Telegram kuwa vikosi vya Kyiv vimepiga hatua fulani eneo la kaskazini na kusini mwa Bakhmut na kwamba vikosi vya Urusi, ambavyo vinadai kuunyakua mji huo, vimeendelea tu kujiimarisha kwenye maeneo wanayoyadhibiti.

Soma pia; Yanayojiri Ukraine: Mashambulizi yaripotiwa Belgorod

Urusi imesema imeanzisha uchunguzi kuhusu vitendo vya kigaidi baada ya shambulio la kuvuka mpaka hapo jana katika eneo lake la Belgorod na kuyashutumu makundi yenye silaha ya Ukraine kuhusika na shambulio hilo. Tuhma zinazokanushwa na Kiev.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW