1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yasema haihusiki na kifo cha Prigozhin

24 Agosti 2023

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema Alhamis taifa lake halihusiki na kifo cha mkuu wa kundi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, katika ajali ya ndege na badala yake ameinyoshea kidole Urusi kwa kuhusika na kifo hicho.

Ukraine | Unabhängigkeitstag in Kiew | Wolodymyr Selenskyj
Picha: kyodo/dpa/picture alliance

Zelensky amesema hayo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa pamoja na rais wa Ureno, Marcelo Rebelo de Soussa, mjini Kyiv.

Ndege aliyokuwamo Prigozhin ilianguka kati ya Moscow na St. Petesburg jana Jumatano, na kuibua uvumi kwamba kiongozi huyo ameuawa.

Katika hatua nyingine, Rais Gitanas Nauseda wa Lithuania amesema mchana wa leo kwamba taarifa hizo haziwezi kuimarisha kwa namna yoyote usalama wa kikanda akionya kuwa bado wapiganaji wa Wagner wapo nchini Belarus.

Ikulu ya Kremlin na wizara wa ulinzi ya Urusi zimeendelea kuwa kimya licha ya kunyooshewa kidole kifo cha Prigozhin.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW