1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ukraine yasema imedungua droni 28 na makombora 4 ya Urusi

25 Septemba 2024

Jeshi la anga la Ukraine limesema leo kuwa limedungua droni 28 kati ya 32 na makombora manne kati ya manane wakati wa shambulizi la usiku kucha la Urusi.

Athari za shambulizi la Urusi mkoani Donetsk
Askari wa zima moto akizima moto kwenye jengo lililoharibiwa baada ya shambulio la Urusi katika mkoa wa Donetsk nchini Ukraine.Picha: Ukraine National Police via AP/picture alliance

Jeshi la anga la Ukraine limesema leo kuwa limedungua droni 28 kati ya 32 na makombora manne kati ya manane wakati wa shambulizi la usiku kucha la Urusi.

Jeshi hilo limesema kuwa Urusi ilirusha makombora manne katika eneo la kusini la Odesa huku gavana wa eneo hilo Ole Kiper akisema kombora moja limelenga eneo la wazi na kusababisha moto ambao umezimwa kufikia sasa.Urusi yaushambulia tena mji wa Kharkiv

Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegram, Kiper ameongeza kuwa vifusi vya droni hizo viliharibu malori mawili bila ya kusababisha majeruhi.

Gavana wa eneo la Kyiv Ruslan Kravchenko amesema shambulizi la droni katika eneo hilo halikusababisha uharibifu kwa miundo mbinu muhimu ya makazi.

Wakati huo huo, mashambulizi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Kharkiv mapema leo yaliharibu jengo kubwa linalotumika kuegesha ndege.