1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yashambulia kituo cha mafuta katika eneo la Crimea

7 Oktoba 2024

Ukraine imesema mapema Jumatatu kwamba vikosi vyake vimekishambulia kituo cha mafuta katika eneo la Crimea linalodhibitiwa na Urusi tangu mwaka 2014.

Urusi | Feodosia
Moshi ukifuka katika kituo cha mafuta kufuatia shambulizi la Ukraine katika mji wa pwania wa Feodosia, kusinimashariki mwa CrimeaPicha: Sergei Malgavko/TASS/dpa/picture alliance

Kyiv imeongeza mashambulizi yanayolenga sekta ya nishati ya Urusi katika miezi ya hivi karibuni ikiamini kwamba maeneo hayo ndiyo yanaipatia Urusi jeuri ya mapato na kuendeleza uvamizi wake nchini Ukraine ambao unapindukia mwaka wa tatu.

Mamlaka zilizowekwa na Urusi huko Crimea zilisema shambulizi lilisababisha kuzuka kwa moto katika ghala la mafuta katika mji wa bandari wa Bahari Nyeusi wenye watu 70,000 lakini hakukuwa na majeruhi walioripotiwa.

Wizara ya ulinzi ya Urusi wakati huohuo ilisema kuwa droni 12 kati ya 21 za Ukraine zilizorushwa usiku kucha zilidunguliwa.

Ukraine imesema mashambulizi hayo ni kisasi cha haki kwa mashambulizi ya Urusi kwenye miundombinu yake ya nishati ambayo yamewaingiza mamilioni gizani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW