1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yasema imezima shambulio kubwa la Urusi

19 Mei 2023

Kikosi cha anga cha jeshi la Ukraine kimesema kimezuwia shambulizi jengine la Urusi nchini humo mapema leo asubuhi kwa kuzidungua ndege 19 zisizokuwa na rubani pamoja na makombora kati ya 28 yaliyovurumishwa nchini humo.

Mabaki ya kombora la Urusi
Mabaki ya kombora la Urusi Picha: Alex Babenko/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa jeshi hilo Yuriy Ihnat ameiambia televisheni ya Ukraine kwamba makombora matatu yaliyorushwa kutoka Bahari Nyeusi pamoja na ndege hizo 16 zililengwa huku akidai mashambulizi kutoka Urusi yanaendelea kila siku.

Urusi imezidisha mashambulizi yake dhidi ya taifa hilo mwezi huu, ambapo Kiev inasema hilo linatokana na Moscow kuogopa mashambulio yanayotarajiwa kufanywa na Ukraine kujibu uvamizi ulioanzishwa na jirani yake huyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW