1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yasema Ujerumani itaipatia makombora ya Taurus

26 Agosti 2023

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksii Reznikov amesema ana imani kwamba Ujerumani itaipatia nchi yake makombora aina ya Taurus.

Taurus Marschflugkörper auf der ILA 2006
Picha: Gemeinfrei

Katika mahojiano aliyofanyiwa na wahariri wa magazeti ya ujerumani ya Bild, Welt na tovuti ya Politico, Reznikov hakufafanua ni lini hasa Makombora hayo yatafikishwa Ukraine, lakini akasema hadhani kama itachukua mwaka mzima kwa hilo kufanyika. 

Ukraine imekuwa ikiiomba Ujerumani kuipa silaha hizo.

Kyiv yaiomba Ujerumani kuipa makombora ya Taurus

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekuwa na mashaka ya kuchuku hatua hiyo, kufuatia hofu kwamba makombora hayo yaliyo na uwezo wa kwenda umbali wa kilomita 500 huenda yakaiwezesha Ukraine kulishambulia eneo la Urusi. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW