Ukraine: Raia wetu takriban 13,500 wamerejea kutoka Urusi
24 Novemba 2023Matangazo
Raia hao wameingia kupitia eneo la Summy mashariki mwa Ukraine na idadi hiyo inawajumuisha watoto 1,653 na watu 131 wenye ulemavu. Moscow imeshutumiwa mara kadhaa kwa kuwahamisha kwa nguvu maelfu ya raia wa Ukraine hadi nchini Urusi.
Kyiv inasema imeorodhesha takriban watoto 20,000 ambao walipelekwa Urusi baada ya Moscow kuanzisha uvamizi wake nchini humo Februari mwaka jana.
Soma pia: Urusi yaendeleza mashambulizi mashariki mwa Ukraine
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC ilitoa mwaka huu waranti wa kukamatwa rais Vladimir Putin kutokana na harakati haramuya kuwahamisha watoto kutoka katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.