SiasaUkraine
Jeshi la Ukraine ladungua droni 35 kazi ya 39 za Urusi
10 Machi 2024Matangazo
Jeshi hilo la Ukrain limesema kupitia ukurasa wa Telegram kwamba droni nyingi ziliharibiwa katika eneo la mashariki mwa Ukraine na kwenye mikoa ya kusini, ingawa haikuelezea kama kulitokea athari zozote.
Aidha limesema, Urusi ilifyatua makombora ya S-300 ingawa halikuweka wazi kama makombora hayo yalifika kwenye maeneo yaliyolengwa.
Taarifa nyingine kutoka mjini Kyiv hii leo zimesema shambulizi la Urusi katika mji wa Myrnograd, ulioko Donesk mashariki mwa taifa hilo limejeruhi karibu watu 9.