1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yasema Urusi imeishambulia meli ya mizigo ya kiraia

5 Machi 2026

Ukraine inasema Urusi imeshambulia kwa droni meli ya mizigo ya kiraia katika bandari ya Chornomorsk kwenye Bahari Nyeusi.

Meli iliyoshambuliwa katika Bahari Nyeusi
Meli iliyoshambuliwa katika Bahari NyeusiPicha: Veysel Altun/Anadolu/picture alliance

Mashambulizi hayo yamefanyika usiku wa kuamkia Alhamis.

Kulingana na gavana wa kijeshi wa Odesa Oleg Kiper, mabaharia kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi hilo.

Kiper ambaye hakutoa idadi ya waliojeruhiwa amesema kuwa meli hiyo ilikuwa inasafirisha mahindi. Urusi ambayo imepinga kuwalenga raia, imetahadharisha kuwa meli yoyote inayoelekea katika bandari za Ukraine, itachukuliwa kama inayobeba mizigo ya kijeshi.

Haya yanafanyika wakati ambapo angalau watu watano wamejruhiwa katika mashambulizi mawili ya Urusi yanayolenga miundo mbinu ya reli kusini mwa Ukraine.

Kulingana na maafisa wa Ukraine, mfanyakazi wa reli alijeruhiwa baada ya droni kuipiga treni ambayo ilikuwa haina abiria mwendo wa asubuhi katika eneo la Mykolaiv.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW