1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yasema uwezo wa angani wa Urusi ni tatizo kubwa

3 Julai 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ukraine Dmytro Kuleba amesema uwezo mkubwa wa Urusi angani ni moja ya matatizo yanayoikumba operesheni ya nchi yake ya kuyakomboa maeneo yaliyokamatwa.

Russland Russische Luftverteidigung Suchoi Su-27 Kampfjet
Picha: Vitaly Timkiv/Sputnik/dpa/picture alliance

Kuleba amedokeza kuwa wanajeshi wa Ukraine wanakumbwa na matatizo wakati Urusi ikiimarisha ngome zake kwa kuchimba mitaro mirefu na kutega mabomu ya ardhini.

Akibainisha kuwa washirika wa Ukraine wa Magharibi wangeweza kuamua mapema kupeleka ndege za kivita, Kuleba amesema sasa anataka waharakishe utoaji wa ndege hizo.

Waziri huyo pia amekosoa matamshi juu ya kushindwa kupiga hatua katika operesheni yao ya kujibu mashambulizi.

Soma pia:London: Vita nchini Ukraine ni changamoto ya kipekee kwa sekta ya anga ya Urusi. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema mwishoni mwa wiki kuwa jaribio la uasi la mkuu wa kampuni ya mamluki wa Wagner nchini Urusi wiki iliyopita huenda likaifaidi operesheni ya Ukraine katika hatua za mwanzo.

Alisema operesheni hiyo haitofanywa haraka kwa sababu anathamini maisha ya binaadamu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW