1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine: Droni zilizodunguliwa zaharibu miundombinu muhimu

25 Oktoba 2023

Maafisa nchini Ukraine wamesema shambulizi la droni la Urusi usiku wa kuamkia leo, dhidi ya eneo la Khmelnytskiy magharibi mwa nchi hiyo, limeharibu mojawapo ya miundombinu muhimu.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Presidential Office of Ukraine/SvenSimon/picture alliance

Sehiy Tiurin, afisa wa ngazi ya juu katika jimbo la Khmeinytskiy amesema kufuatia kudunguliwa kwa droni za Urusi, vifusi vilianguka kwenye miundombinu muhimu katika wilaya ya Shepetivka, na kuharibu majengo wanakoishi watu, na pia magari.

Ameongeza kwamba takriban watu 16 walitafuta matibabu baada ya kujeruhiwa.

Jeshi la Ukraine lilisema kupitia ukurasa wake wa Facebook kwamba vikosi vyake vya angani vilidungua droni zote 11 za Urusi zilizorushwa usiku.

Soma pia:Ukraine yadungua droni na makombora yaliyorushwa na Urusi

Kwingineko, waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amefanya ziara ya nadra eneo la mapambano nchini Ukraine kuwatembelea wanajeshi wake na kufanya mkutano nao kwenye eneo maalum la kijeshi.

Hayo yamethibitishwa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi kwenye ukurasa wake wa telegram.

Hata hivyo haikubainika wazi ikiwa kweli eneo hilo alikozuru liko ndani ya mipaka ya Ukraine.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW