1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine: Wanajeshi wa Korea Kaskazini kuanza vita karibuni

Angela Mdungu
25 Oktoba 2024

Duru za kijasusi za Ukraine zimedai kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini huenda wakaanza kutumiwa na Urusi katika vita vya Ukraine mwishoni mwa juma hili.

Wanajeshi wanaoshukiwa kuwa wa Korea Kaskazini nchini Urusi
Televisheni inaonyesha wanajeshi wanaohisiwa kutoka Korea Kaskazini wakiwa wamesimama kwenye foleni kupokea vifaa kutoka Urusi Oktoba. 21, 2024.Picha: Ahn Young-joon/AP/picture alliance

Rais VolodymyrZelensky amesema taarifa za kiintelijensia za nchi hiyo, zimebaini kwamba kundi la kwanza la wanajeshi wa Korea Kaskazini wataanza kutumika katika vita hivyo kati ya Jumapili na Jumatatu. Nchi za Magharibi zimeonya kuwa hatua kama hiyo itachochea zaidi vita hivyo vya takriban miaka mitatu na kuleta athari kubwa katika siasa za kikanda. Kwa mujibu wa kurugenzi kuu ya intelijensia ya Ukraine, vikosi vya Korea Kaskazini vilionekana tangu siku ya Jumatano mkoani Kursk. Wanajeshi wake walikuwa wakipata mafunzo kwa wiki kadhaa katika kambi mashariki mwa Urusi. Inakadiridiwa kuwa wanajeshi wapatao 12,000 wametumwa na Pyongyang nchini Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW