1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine: Wanajeshi wa Urusi wamepata mafanikio mjini Bakhmut

30 Machi 2023

Maafisa wa kijeshi wa Ukraine wamesema wanajeshi wa Urusi wamepata mafanikio fulani katika uwanja wa mapambano wa mji wa mashariki wa Bakhmut.

Wolodymyr Selenskyj
Picha: PRESIDENT OF UKRAINE OFFICE/APA/IMAGO

Hata hivyo maafisa hao wamesema askari wa Ukraine wanaendelea kuhimili kishindo katika mapambano ambayo yamedumu kwa miezi kadhaa ambapo pande zote zimepata hasara kubwa. 

Katika upande wa kusini mwa Ukraine, Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Nishati ya Atomiki - IAEA Rafael Grossi amesema kumekuwa na mkusanyiko mkubwa wa wanajeshi katika eneo la kiwanda cha nishati ya nyuklia kinachodhibitiwa na Urusi cha Zaporizhzhia na hakiwezi kulindwa.

Ukraine:Urusi yapambana kukamata udhibiti kamili Bakhmut

Naibu Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Ryabkov amesema leo kuwa Moscow bado inafanya mazungumzo na mkuu huyo wa IAEA kuhusu wazo la kuweka eneo salama karibu na kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW