1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yashambulia kiwanda cha kusafisha mafuta Urusi

26 Septemba 2025

Ukraine imeendeleza mashambulizi yake ya kimfumo dhidi ya sekta ya mafuta ya Urusi ikilenga kiwanda cha kusafisha mafuta katika eneo la kusini. Haya ni kulingana na mamlaka ya Urusi.

Urusi Rostow am Don 2022 | Moto uliosababishwa na shambulizi la droni la Ukraine
Shambulizi la droni la Ukraine dhidi ya kiwanda cha mafuta cha Novoshakhtinsk nchini UrusiPicha: Russian Emergency Ministry Press Service/AP Photo/picture alliance

Mamlaka hiyo ya Urusi katika eneo la Krasnodar, imeripoti kuzuka kwa moto mdogo kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta cha Afipski na kusema sehemu za droni moja ziliangukia kiwanda hicho.

Hata hivyo wamesema hakukuwa na majeruhi.

Kulingana na vyanzo Ukraine, kiwanda hicho kinachozalisha petroli na dizeli, awali kilishambuliwa mnamo Agosti 28.

Wataalamu wanakadiria kuwa Urusi imepoteza takriban robo ya uwezo wake wa usindikaji kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya viwanda vya kusafisha mafuta, vituo vya mafuta na vya upakiaji.

Hali hii imesababisha uhaba wa dizeli na petroli katika baadhi ya mikoa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW