1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yashambulia miundo mbinu ya nishati ya Urusi

29 Oktoba 2025

Ukraine imeshambulia miundo mbinu ya nishati ya Urusi kwa droni na kutatiza usafiri wa anga kote nchini humo pamoja na kufanya mashambulizi kuelekea mji mkuu wa nchini hiyo Moscow kwa siku ya tatu mfululizo.

Ukraine  Kharkhiv 2025 | Maafisa wa msaada
Maafisa wa uokoaji kwenye eneo la shambulizi la Urusi nchini UkrainePicha: Vyacheslav Madiyevskyy/REUTERS

Katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wa Telegram, gavana wa rasi ya Crimea, aliyechaguliwa na Urusi Sergei Aksyonov, amesema chombo kilichokuwa kimehifadhi mafuta mjini Simferopol kilishambuliwa na droni ya Ukraine na kushika moto.

Hata hivyo amesema hakuna vifo vilivyoripotiwa huku huduma za dharura zikifanya kazi katika eneo hilo.

Wakati huo huo, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kupitia ujumbe kwenye mtandao wa Telegram kwamba vikosi vyake ya ulinzi wa anga vilidungua takriban droni 100 za Ukraine usiku kucha ikiwa ni pamoja na sita kwenye eneo la Moscow na nyingine kwenye maeneo 11 ya rasi hiyo ya Crimea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW