1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yashambulia uwanja wa ndege wa kijeshi huko Crimea

21 Septemba 2023

Ukraine imesema imeushambulia uwanja wa ndege wa kijeshi karibu na mji wa Saky unaoshikiliwa na Urusi kwenye rasi ya Crimea.

Krim Sewastopol Großbrand in Erdöl-Lager
Picha: MIKHAIL RAZVOZHAEV/TELEGRAM/REUTERS

Hili ni shambulio la hivi punde linalodaiwa kutekelezwa katika eneo hilo la Bahari Nyeusi ambalo Kiev imeapa kulidhibiti tena. 

Chanzo cha habari katika kitengo cha usalama cha Ukraine kimesema kuwa mashambulizi hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa vifaa vya Urusi, hasa ikizingatiwa kuwa, wakati wa mashambulizi hayo, kulikuwepo katika uwanja huo karibu dazeni ya ndege za kivita na mifumo ya ulinzi ya Urusi.

Urusi na Ukraine zashambuliana usiku wa kuamkia leo

Mamlaka za Urusi eneo hilo zimekanusha mara moja taarifa hizo na kusema kuwa mifumo yao ya anga ilizima mashambulizi hayo kwa kudungua ndege zote zisizo na rubani zilizorushwa na Ukraine.

Moscow iliinyakua kinyume cha sheria rasi ya Crimea mnamo mwaka 2014.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW