1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yasikitishwa na kuvunjika uhusiano na Niger

8 Agosti 2024

Ukraine imesema leo kuwa imesikitishwa na uamuzi wa Niger kuvunja mahusiano ya kidiplomasia.

Mataifa matatu ya Niger, Mali na Burkina Faso yanaongozwa na watawala wa kijeshi
Mataifa matatu ya Niger, Mali na Burkina Faso yanaongozwa na watawala wa kijeshi.Picha: Mahamadou Hamidou/REUTERS

Niger ilichukua uamuzi huo siku chache tu baada ya nchi jirani Mali kuchukua uamuzi sawa na huo ikivituhumu vikosi vya Ukraine kwa kuyaunga mkono makundi ya waasi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Niger na Mali zinaendeshwa na serikali za kijeshi ambazo ziliingia madarakani katika mapinduzi ya karibuni na zimeigeukia Urusi na kundi lake la mamluki wa Wagner kwa msaada.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Ukraine imesema katika taarifa kuwa inasikitisha kuwa maafisa wa Niger wamechukua uamuzi huo wa kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Ukraine bila kufanya uchunguzi wowote kuhusu tukio la nchini Mali na bila kutoa ushahiri wowote kuhusiana na sababu za hatua ya aina hiyo.

Mali ilisema Kyiv iliwapa wanajeshi waasi taarifa za intelijensia, ambao kisha walizitumia kuwauwa mamluko kutoka kundi la mamluki wa Wagner na askari wa Mali kwenye uwanja wa mapambano mwezi uliopita wa Julai.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW