1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yasisitiza kuwa mwanachama wa NATO

3 Desemba 2024

Ukraine imesisitiza kwamba kupata uanachama wa jumuiya ya NATO ndio hatua pekee itakayotowa hakikisho la kweli la usalama wake.

Brussels
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Picha: Remko de Waal /ANP/IMAGO

Kauli ya Ukraine imejiri wakati mawaziri wa kigeni wa Jumuiya ya NATO wamejiandaa kulikataa shinikizo la Kyiv la kutaka kukaribishwa kuwa mwanachama wa Jumuiya hiyo, kabla Donald Trump hajaingia madarakani nchini Marekani.

Trump ameahidi kushinikiza hatua ya kufikiwa makubaliano ya haraka ya kumaliza vita vya Urusi, hatua ambayo inaifanya serikali mjini Kiev kuhangaika kutafuta msimamo wake kabla ya utawala huo mpya Marekani.

Rais Zelensky aitaka Marekani iushawishi Umoja wa Ulaya ukubali kuikaribisha Ukraine NATO

Wanadiplomasia wamesema hakuna uwezekano wa mkutano huo wa Brussels wa mawaziri wa kigeni wa NATO kukubali pendekezo la Ukraine.

Marekani na Ujerumani zimeshajitenga na pendekezo hilo kwa kukhofia linaweza kusababisha muungano huo kutumbukia vitani na Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW