1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yataka juhudi zaidi za kuleta amani zifanyike

5 Agosti 2023

Maafisa waandamizi kutoka nchi takriban 40 zikiwemo Marekani, China na India wanashiriki kwenye mazungumzo ya kutafuta amani ya Ukraine yanayofanyika Saudi Arabia.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Pool Philip Reynaers/belga/dpa/picture alliance

Ukraine na washirika wake wanatumai mazungumzo hayo yataelekea kwenye makubaliano juu ya kanuni muhimu za kukomesha vita nchini humo. Mkutano huo wa siku mbili ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia za Ukraine za kutafuta kuungwa mkono nje ya washirika wake wa msingi na kuzishikirisha nchi za kusini mwa dunia ambazo zimesitasita kuunga mkono upande mmoja katika mzozo ambao umeathiri uchumi wa dunia. Urusi haishiriki, ingawa imesema itaufuatilia mkutano huo.

Soma zaidi: Saudi Arabia yaandaa mazungumzo ya kumaliza vita vya Ukraine

Maafisa wa Urusi, Ukraine na wa kimataifa wanasema hakuna matarajio ya kufanyika mazungumzo ya ana kwa ana ya amani kati ya Ukraine na Urusi kwa sasa wakati vita vinaendelea. Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky amesema anatumai mkutano wa nchini Saudi Arabia utaweka msingi wa mkutano wa kilele wa viongozi wa dunia watakaounga mkono mpango wake juu ya kuleta amani. Kulingana na mpango huo, Urusi inatakiwa irudishe sehemu zote za Ukraine inazozikalia na iyaondoe majeshi yake kutoka Ukraine.  

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW