1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yataka meli za Urusi zikamatwe na mataifa ya EU

29 Januari 2026

Mjumbe maalum wa Ukraine kuhusu vikwazo amewataka viongozi wa Ulaya kutokhofia kuzikamata meli za Urusi ili kuizuia kukwepa vikwazo vya nchi za Magharibi

Ukraine imeutaka Umoja wa Ulaya kutokhofia kuchukuwa hatua za kutumia nguvu dhidi ya meli za Urusi ikitowa mfano wa kile kilichofanyika kwa meli za mafuta za Venezuela ambazo baadhi zilizohusishwa na Urusi zilizokamatwa na Marekani.

Mjumbe maalum wa rais Zelensky kuhusu vikwazo, Vladyslav Vlasiuk ambaye ameitembelea Ujerumani, amesema kwamba kazi pia inahitaji kufanyika  kuhakikisha vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi dhidi ya Urusi vinazingatiwa.

Zelensky: Trump na Marekani wanaweza kumaliza vita Ukraine

Mjumbe maalum wa Ukraine Vlasiuk amesema anaamini  ikiwa baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya zitaanza kuchukuwa hatua za kuzikamata meli za Urusi, Moscow haiwezi kufanya chochote, lakini pia ameonesha dhamira ya Kiev ya kutaka kuhakikisha kiwango cha usafirishaji mafuta cha Urusi kinapunguzwa kwa asilimia hadi 20.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW