1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yateua naibu waziri mpya wa mambo ya ndani

18 Januari 2023

Serikali ya Ukraine imemteua mkuu wa jeshi la polisi Ihor Klymenko kukaimu nafasi ya naibu waziri wa mambo ya ndani baada ya aliyekuweko kuuwawa kwenye ajali ya helikopta

Ukraine | Absturz Militärflugzeug AN-26
Picha: Sergey Bobok/AFP

Serikali ya Ukraine imemteua mkuu wa jeshi la polisi Ihor Klymenko kukaimu nafasi iliyoachwa na  naibu waziri wa mambo ya ndani aliyefariki kwenye ajali ya helikopta hii leo.

 Waziri mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal  ametangaza uteuzi huo wa naibu waziri wa mambo ya ndani saa chache baada ya kuthibitika aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Denys Monastyskyi ameuwawa kwenye ajali ya Helikopta iliyoanguka karibu na mji mkuu Kiev.

Picha: Igor Burdyga/DW

Mkuu wa jeshi la polisi Ihor Klymenko sasa anachukuwa nafasi hiyo  na ameshasema kwamba atatekeleza majukumu ya waziri.

Lakini huko Urusi nako rais Vladmir Putin amesema hana mashaka kwamba nchi yake itaondoka na ushindi kwenye vita nchini Ukraine  licha ya jeshi lake kukabiliwa na hujuma katika operesheni yake hiyo ya kijeshi ya takriban mwaka mzima.

Putin ametowa kauli hiyo leo wakati akizungumza mbele ya wafanyakazi katika kiwanda kimoja cha silaha  kilichoko katika mji wa pili kwa ukubwa wa St Petersburg nchini humo.

Picha: Mikhail Klimentyev/dpa/picture alliance

Ameweka wazi kwamba licha ya jeshi lake kushindwa mara kadhaa kwenye mapambano hayo,ushindi ni jambo la lazima na hana mashaka kuhusu hilo.

Wakati rais Vladmir Putin akitowa msimamo huo mjini Brussels naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Mircea Geoana ameitahadharisha jumuiya hiyo kwamba inapaswa kujiweka tayari kutokana na hatua ya Urusi ya kujiandaa kuendeleza vita.

Amesema NATO inapaswa kuiunga mkono Ukraine kwa namna yoyote.Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa kijeshi wa jumuiya hiyo kutoka nchi za Ulaya amesema nchi wanachama wa jumuiya hiyo zinabidi kuwekeza zaidi  katika ulinzi ,kuongeza uzalishaji silaha na kutafuta  teknolojia mpya kujiandaa na vita vya baadae.NATO, EU zaapa uungaji mkono zaidi kwa Ukraine

Wakuu wa majeshi wa NATO wanatarajiwa kujadili namna washirika hao wanavyoweza kutanua hatua ya kupeleka silaha,kutoa mafunzo na kuiunga mkono Ukraine katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo.

Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Lakini pia wakati huohuo nchini Ukraine kumeshuhudiwa ziara ya waziri wa ulinzi wa Canada Anita Anand aliyetembelea Kiev na kukutana na maafisa wa Ukraine hii leo pamoja na kutangaza nchi yake itaipelekea Ukraine magari 200 makubwa ya kijeshi yanayotumika vitani kusafirisha watu, ikiwa kama sehemu ya mpango mpya wa msaada msaada wake wa kijeshi.

Ukraine yaomba msaada zaidi wa kijeshiMsaada huo unagharimu zaidi ya dola milioni 90 na unatolewa kama sehemu ya msaada wa ziada wa kijeshi wa  dola milioni 500 uliotangazwa na waziri mkuu Trudeau Novemba mwaka jana. Kwa mujibu wa Canada magari hayo yanapelekwa Ukraine kufuatia ombi la nchi hiyo.