1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yaushambulia mji mkuu wa Urusi kwa droni

21 Agosti 2024

Maafisa nchini Urusi wanasema Ukraine imeishambulia nchi hiyo kwa msururu wa ndege zisizokuwa na rubani leo, huku mifumo ya ulinzi wa angani ikiziharibu droni tatu.

Mashambulizi katika Shule ya Urusi huko Bryansk
Huduma za dharura kwenye jumba la mazoezi ambapo kulitokea mashambulizi.Picha: Nadezhda Mikheyeva/TASS/dpa/picture alliance

Droni hizo zimeharibiwa kilomita 38 kusini mwa Kremlin na zengine 15 zikaharibiwa katika mpaka wa eneo la Bryansk. Meya wa Mji Mkuu wa Urusi, Moscow, Sergei Sobyanin amesema droni hizo tatu zilizokuwa zimerushwa kuelekea Moscow, zilidunguliwa katika mji wa Podolsk. Haijawa wazi bado ni droni ngapi ambazo zimerushwa na Ukraine. Huku hayo yakiarifiwa, Urusi sasa inasema kwamba uvamizi wa Ukraine katika eneo la Kursk huko Urusi, ulipangwa kwa ushirikiano wa taarifa za kijasusi za Marekani, Uingereza na Poland. Haya yameripotiwa katika gazeti la Urusi la Izvestia. Huduma ya Intelijensia za Kigeni nchini Urusi imeliambia gazeti hilo kwmaba ina "taarifa za kuaminika" kuhusiana na jambo hilo, ila haikutoa ushahidi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW