1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yashambulia uwanja wa ndege wa kijeshi Urusi

Angela Mdungu
20 Oktoba 2024

Vikosi vya Ukraine vimeshambulia miundombinu ya kijeshi katika uwanja wa ndege wa jeshi la Urusi kwenye mkoa wa Lipetsk, kwa mujibu wa Mkuu wa Majeshi wa Kyiv.

Moscow, Urusi
Moshi ukifuka Moscow baada ya Urusi kuidungua droni ya UkrainePicha: Ostorozhno Novosti/REUTERS

Taarifa hiyo imesema jeshi hilo lilishambulia pia kiwanda cha kutengeneza mabomu kilicho mkoa wa Nizhny Novgorod. Ripoti hizo zimethibitishwa baada ya maafisa wa Urusi na Chaneli za jukwaa la telegram kuripoti kuwa Ukraine iliilenga mikoa hiyo katika mashambulizi ya droni yaliyofanywa usiku wa kuamkia jumapili.

Hayo yanajiri wakati jeshi la ulinzi wa anga la Urusi liliripoti kuwa lilizidungua droni 110 katika maeneo kadhaa ya Ukraine ikiwemo moja huko Moscow. Droni 43 zilidunguliwa katika mkoa wa Kursk ulio mpakani na nyingine 27 zilizoangushwa katika mkoa wa Kusini magharibi wa Lipetsk.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW