1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Droni 34 kati ya 55 za Urusi zadunguliwa Ukraine

Angela Mdungu
16 Januari 2025

Jeshi la Ukraine limearifu kwamba limefanikiwa kuzidungua ndege 34 zisizo na rubani kati ya 55 zilizorushwa na Urusi usiku wa kuamkia lAlhamisi. Miundombinu ya nishati imeripotiwa kuharibiwa na mashambulizi hayo.

Mashambulizi ya droni katika anga la Ukraine
Mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine ukizuia droni za UrusiPicha: Evgeniy Maloletka/AP/picture alliance

Kwa mujibu wa mamlaka za ndani za Ukraine, mabaki ya ndege hizo zisizo na rubani yaliharibu miundombinu ya nishati katika mkoa wa Poltava na kusababisha watu 300 wakose huduma ya umeme.

Katika kipindi cha miezi kadhaa ya hivi karibuni, Urusi imekuwa ikirusha mkururo wa droni karibu kila usiku kuelekea Ukraine hali inayoilazimu Kyiv kutumia rasilimali za gharama kubwa katika kukabiliana nazo.

Katika hatua nyingine Urusi na Ukraine zimebadilishana wafungwa wa vita , mchakato uliofanyika chini ya msaada wa Umoja wa Falme za Kiarabu. Nchi hizo mbili zenye mzozo, kila moja imewaachilia wafungwa 25.

Soma zaidi: Urusi yavurumisha wimbi la mashambulizi kuelekea Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibithisha hatua hiyo ya kubadilishana wafungwa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Telegram.

Licha ya hatua hiyo, jeshi la Ukraine limearifu kuwa limewakamata zaidi ya wapiganaji 27 wa Urusi katika mkoa wa Kursk ambako majeshi ya Urusi na Ukraine yanapambana tangu mwezi Agosti mwaka uliopita. Jeshi hilo imesema kuwa wanajeshi wa Moscow waliokamatwa wanatoka katika mikoa kadhaa ya Urusi pamoja na rasi ya Krimea iliyonyakuliwa na Urusi tangu mwaka 2014.

Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Remko de Waal /ANP/IMAGO

Zelensky azungumza na Rais Duda wa Poland

Hayo yanaendelea wakati Rais Volodymyr Zelenky akiwa ziarani Poland ambako amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Andrzej Duda. Mazungumzo hayo yaliyofanyika Jumatano jioni yalilenga kuzungumzia uwezekano wa kurejesha amani Ukraine  pamoja na suala la mauaji ya raia wa Poland yaliyofanywa wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.

Kwa upande wake Rais Duda wa Poland amesema mazungumzo kuhusu suala hilo yanafanyika chini ya usimamizi wa serikali inayoundwa na muungano wa vyama nchini humo pamoja na Wizara ya Utamaduni ya Ukraine kuhusu raia hao wa Poland waliouwawa katika vita vya pili vya dunia kwenye eno ambalo sasa ni sehemu ya Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW