1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Droni 62 kati ya 45 za Urusi zadunguliwa Ukraine

Angela Mdungu
10 Novemba 2024

Jeshi la anga la Ukraine mapema leo limesema limezidungua droni 62 kati ya 145 zilizorushwa na Urusi nchini humo. Limesema halifahamu droni 67 zilikoangukia wakati 10 zilielekea upande wa Urusi, Moldova na Belarus.

Urusi na Ukraine zimeendelea kushambuliana kwa droni
Juhudi za kuzima moto katika mkoa wa Odesa baada ya mashambulizi ya droni ya UrusiPicha: STATE EMERGENCY SERVICE OF UKRAINE/REUTERS

Maafisa wa Ukraine wamesema watu wawili wamejeruhiwa katika mkoa wa Odesa kutokana na mashambulizi hayo. 

Urusi kwa upande wake imesema imeziangamiza droni 70 za Ukraine zikiwemo 34 zilizoilenga Moscow katika moja ya mashambulizi makubwa katika mji huo mkuu tangu mzozo huo ulipoanza mwaka 2022.

Soma zaidi: Urusi yafanya mashambulizi ya usiku kucha nchini Ukraine

Meya wa mji huo Sergei Sobyanin amebainisha kuwa nyingi kati ya droni zilizorushwa na Ukraine zilikuwa zikielekea katika maeneo ya Ramenskoye na Domodedovo kusini mwa Moscow. Mamlaka za viwanja vya ndege zimesema mashambulizi hayo yalisababisha kusitishwa kwa safari za ndege viwanja vya Domodedovona Zhukovsk.

Soma zaidi: Mashambulizi ya droni ya Urusi yaharibu miundombinu muhimu ya Ukraine

Mashambulizi hayo yamefanywa walkati Urusi ikiwa mwenyeji wa wanadiplomasia na maafisa wa ngazi ya juu kutoka mataifa 50 ya Afrika huko Sochi kwenye mkutano wa juu ya ushirikiano kati ya Moscow na bara hilo.