1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaushambulia mji wa Kharkiv wa Ukraine mfululizo

3 Aprili 2026

Mamlaka katika mji wa Kharkiv mashariki mwa Ukraine imesema leo kuwa mji huo umeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya anga ya mfululizo kutoka Urusi kwa zaidi ya siku moja sasa.

UkraineI Kharkiv 2026
Zimamoto mjini Kharkiv, Ukraine wakipambana kuuzima moto uliotokana na shambulio la UrusiPicha: Sofiia Gatilova/REUTERS

Mamlaka katika mji wa Kharkiv mashariki mwa Ukraine imesema leo kuwa mji huo umeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya anga ya mfululizo kutoka Urusi kwa zaidi ya siku moja sasa.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram, gavana wa kijeshi wa mji huo, Oleh Syniehubov, ameandika kwamba mashambulizi ya makombora na droni yaliyoulenga mji huo yamejeruhi na kuharibu majengo ya makaazi na ofisi.

Mji huo ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, ulikuwa na idadi ya watu milioni 1.4 kabla ya vita, uko umbali wa takriban kilomita 40 tu kutoka mpaka wa Urusi. Kwa mujibu wa mamlaka nchini Ukraine ni kwamba leo siku ya Ijumaa Kuu zinatimia siku 1,500 tangu uvamizi wa Urusi Februari mwaka 2022.

Kwa upande wa Urusi, Wizara ya Ulinzi huko Moscow imeripoti kwamba droni 192 za Ukraine zilidunguliwa siku ya Alhamisi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW