1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Ukuaji wa uchumi barani Afrika huenda ukashuka

10 Aprili 2026

Benki ya Dunia imeonya kiwango cha ukuaji wa uchumi barani Afrika kitashuka 2026 hasa kusini mwa Jangwa la Sahara, tofauti na ilivyokadiriwa awali. Hii inatokana na vita vya Iran ambavyo vimetikisa biashara za mafuta.

Symbolbild Treibstoff & Energie in Ghana
Wataalamu wanaonya kwamba ukuaji wa uchumi barani Afrika huenda ukashuka kufuatia vita vya IranPicha: Bermix/Pond5 Images/IMAGO

Kulingana na ripoti ambayo imetolewa siku ya Jumatano, kupanda kwa bei za mafuta na mbolea hivi karibuni kutokana vita na migogoro katika Mashariki Ya kati kunatishia ukuaji wa uchumi wa bara Afrika.

Itakumbukwa kuwa mataifa mengi ya Afrika ni wategemezi wakubwa wa bidhaa zinazoendesha sekta za uchukuzi na kilimo ambazo ni muhimu sana katika uchumi wa Afrika. Mataifa ambayo yanatarajiwa kuathirika zaidi kutokana na hali hii ni Kenya Ethiopia, Burundi, Malawi na  Mozambique.

Isitoshe, idadi kubwa ya raia wa Afrika wanaofanya kazi katika mataifa ya Mashariki ya Kati hawataweza kutuma nyumbani viwango vilevile vya pesa wanazotuma katika kipindi hiki ambapo biashara ya uwekezaji katika nchi hizo zimo katika msukosuko. Kwa mfano Ethiopia ina wafanyakazi 750,000 katika nchi ya Saudi Arabia pekee na mchango wao kwa uchumi wa taifa lao ni muhimu sana.

Benki ya Dunia inabashiri kuwa tofauti na matarajio ya awali kwamba uchumi wa Afrika ungekuwa kwa asili mia 4.4 mwaka huu, sasa utakuwa kwa asili mia 4.1 tu. Tatizo lingine ni kwamba nchi kadhaa haziwezi kuimudu hali hii kutokana na mzigo mkubwa wa madeni. Mapato mengi ya nchi yanatumiwa kulipa madeni hayo.

Nembo ya Benki Kuu ya Dunia Picha: Rainer Jensen/dpa/picture alliance

Ukuaji wa kiuchumi utaathirika kwa kiasi gani? 

Kwa sasa mataifa kadhaa yanatumia asili mia 18 hivi ya mapato yao kulipa madeni, kiwango ambacho kimepanda katika kipindi cha miaka kumi ambapo mwaka wa 2017 kilikuwa asili mia 9 tu.

Onyo hilo la benki ya dunia linakuja wakati Marekani na Iran zikijiandaa kufanya mazungumzo baada ya kukubaliana kusitisha vita kwa angalau wiki mbili. Kristalina Georgieva ambaye ni mkurugenzi wa shirila la Fedha IMF ametoa angalizo hili

"Swali ni vipi kiwango hicho cha ukuaji kitakavyoathirika. Jibu litategemea muda ambao usitishwaji wa mapigano utadumu, na pili, kiwango cha uharibifu kitakachosababishwa na vita hivi."

Lakini hata katika kipindi hiki cha mazungmzo, hakuna matarajio kuwa bei za mafuta na mbolea zitashuka. Wachumi wanasema badala yake zitandelea kupanda kwani biashara zote katika mnyororo huo zinaendelea kufanyika katika mazingira ya wasiwasi

na mashaka.

Hata hivyo kuna matarajio kuwa nchi za Magharibi mw Afrika zitapata unafuu kutokana na bei ya mbolea.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW