1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukuaji wa uchumi ulimwenguni kupungua mwaka 2023

26 Januari 2023

Umoja wa Mataifa umetabiri ukuaji wa uchumi wa ulimwengu utapungua kwa kiasi kikubwa hadi 1.9% mwaka huu.

IWF Logo, Schild
Picha: Maksym Yemelyanov/Zoonar/picture alliance

Idara ya masuala ya uchumi na masuala ya kijamii ya Umoja wa Mataifa imesema kasi ya ukuaji wa uchumi kwa sasa ulimwenguni imepungua kuanzia mataifa yanayoendelea hadi yaliyoendelea, huku mengi yakikabiliwa na kitisho cha mdororo wa uchumi kwa mwaka huu wa 2023.

Ripoti ya Umoja huo ya kurasa 178 aidha imesema makisio ya ukuaji kwa mwaka huu ya asilimia 1.9, tofauti na asilimia 3 iliyokadiriwa mwaka 2022, ni ya chini mno kushuhudiwa katika miongo ya karibuni.

Hata hivyo imekisia ukuaji wa wastani wa hadi asilimia 2.7 mwaka 2024 ikiwa mfumuko wa bei na mtikisiko wa kiuchumi vitapungua.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW