1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukuta wa Berlin: Jinsi ilivyotokea na unavyoonekana leo

Oumilkheir Hamidou
4 Novemba 2019

November tisa mwaka 1989 vita baridi vilimalizika kati ya tawala za kiimla na zile za kidemokrasi. Chanzo cha hali hiyo ni matukio yaliyojiri nje ya Ujerumani; nchini Poland, Hungary na Urusi au Umoja wa Usovieti.

Deutschland, Brandenburger-Tor
Picha: picture-alliance

Kilikuwa kitambulisho cha kugawika ulimwengu sehemu mbili: Mashariki na mgharibi, kitambulisho cha mapambano kati ya ukoministi na ubepari; Ukuta wa Berlin uliojengwa  mwaka 1961 na viongozi wa kiimla wa jamhuri ya kidemokrasi ya Ujerumani GDR. Sehemu ya magharibi ingawa ilikuwa na ukuta wa seruji na senyenge za vyuma uliokuwa na urefu wa kilomita 155 hata hivyo watu waliweza kupita na kwenda kila mahala. Sehemu ya magharibi ya mji wa Berlin ilikuwa kwa hivyo kisiwa huru kati  ya eneo la kikoministi la GDR.

Badala yake wengi wa wakaazi wa Ujerumani mashariki walikuwa wakiangalia sehemu hiyo iliyokuwa karibu sana  ya magharibi kuwa eneo lisiloweza kufikiwa.

Hali ilibadilika kufumba na kufumbua usiku wa Novemba tisa mwaka 1989, baada ya kituo cha televisheni kutangaza mubashar katika mkutano na waandishi habari kuhussu sheria mpya ya usafiri. Kwa mujibu wa sheria hiyo watu wanaruhusiwa kwenda pia katika nchi za magharibi-tena haapo hapo. Maelfu ya watu wakafunga safari kuelekea vivukio vya ndani vilivyokuwa vikilindwa na jeshi na ambavyo kufumba na kuifdumbuwa vilifunguliwa.

Ukuta wa Berlin, 1989Picha: picture alliance/DB dpa

Picha za watu waliokuwa wakisherehekea katika mji ambao haukuwa tena umegawika zikaenea katika kila pembe ya dunia. Zikadhihirisha kimsingi mwisho wa kugawika Ujerumani. Karibu mwaka mmoja baadae, Oktoba tatu mwaka 1990 nchi hii iliyokuwa imegawika tangu vilipoalizika vita vikuu vya pili vya dunia aikaungana upya. Tukio hilo la kihistoria ulimwenguni limewezekana tu kwakua madola 4 makuu yaliyoshinda vita yalikubaliana: yaani jumuia ya kujihami ya nchi za magharibi; Marekani,Uingereza, Ufaransa na Umoja wa kikoministi wa jamhuri za kijamaa za Usovieti.

Michael GorbatchovPicha: picture-alliance/dpa/A. Scheidemann

Muhimu yalikuwa maridhiano yaliypofikiwa na kiongozi aliyeingia madarakani mwaka 1985 mkoministi mpenda mageuzi Michael Gorbatchov. Muhimu ilikuwa kuingia madarakani Mikhail Gorbatchov mwaka 1985 na sera zake za mageuzi na akuacha milango wazi Glasnost na Perestroika. Kiini cha sera yake na pia siasa yake ya nje ni kuondokana na nadharia ya Breschnev. Bila ya kutilia maana chochote kitakachojiri katika madola ndugu ya kijamaa, mataifa hayo yanabidi yabebe wenyewe majukumu yao. Kwa hivyo Umoja wa jamhuri za usovieti haziotoingilia kati, kama ilivyosghuhudiwa mwaka 1968 mjini Prag, mwaka 1956 nchini Hungary na mwaka 1953 katika GDR pale viongozi wa Umoja wa Usovieti waalipotuma vifaru kukandamiza vuguvugu laa maandamano."

Wanaharakati wa haki za binaadam kataika nchi zote za ulaya ya mashariki walipata moyo na kutaraji kuziona nchin zao pia zikianzisha sera za mageuzi za Glasnost na Perestroika. Nchini Poland vuguvugu la wanahakati wanaoda haki za wafanyakazi Solidarnosvch likaanza kuzungumza na viongozi na kufika hadi ya kuitishwa meza ya duawara ya mazungumzo iliyowakilisha pia kanisa katoliki

Katika nchi nyengine pia wimbi la mageuzi likaanza kupiga. Nchini Hungary serikali ikaanza tangu mwezi May kufungua kambi za mpakani kuelekea Austria. Kwa namna hiyo njia iawa wqazi kati ya Mashariki na magharibi. Mamia ya wajerumani mashariki waliipa kisogo nchi yao kupitia njia hiyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW