Ukuwaji na maharibiko ya Kiswahili
27 Agosti 2014Matangazo
Katika sehemu hii ya mfululizo wa makala za Kiswahili Kina Wenyewe, Mohammed Khelef anazungumza na mwandishi na mtaalamu wa Kiswahili, Prof. Farouk Topan, juu ya dhana ya ukuwaji na mabadiliko ya lugha ya Kiswahili. Je, Kiswahili kinakumbwa na mabadiliko gani kwa sasa? Na je, kukuwa na kubadilika kwa Kiswahili kunamaanisha kuiondoa lugha hiyo kwenye asili yake?
Kusikiliza makala nzima, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Mohammed Khelef
Mhariri: Josephat Charo