1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSenegal

Wahamiaji 600 wakamatwa katika pwani ya Senegal

2 Oktoba 2023

Jeshi la Senegal limesema limefanikiwa kuizua boti zilikuwa na wahamiaji takriban 600, katika opereseni iliyodumu kwa takribani siku tatu.

Senegal | Marine stoppt Schiff mit Migranten
Picha: SENEGALESE NATIONAL NAVY/REUTERS

Wahamiaji hao walikuwa wakielekea katika  mataifa ya Ulaya. Taarifa zinasema katika tukio la kwanza kulikuwa na boti mbili za mbao zilizokuwa na watu 262, wakiwemo watoto 13.

Lakini Alhamis na Ijumaa boti tatu zilikamatwa zikiwa na jumla ya wahamiaji 343. Hata hivyo waokozi hawajataja asili ya wakimbizi hao. Wahamiaji hao wamekabidhiwa kwa mamlaka nchini Senegal.

Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhima na uhamiaji (IOM) linasema katika nusu ya kwanza ya mwaka huu jumla ya wahamiaji 7,213 kutoka Afrika wamewasili katika visiwa hivyo vya Canary.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW