1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya katika zama za Trump, siku ya Kanisa

29 Mei 2017

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanazungumzia ziara ya rais Marekani barani Ulaya, mkutano wa kilele wa mataifa saba yalieondelea kiviwanda G7 na siku ya Kanisa la Kiprotestant ilioadhmishwa nchini Ujerumani.

Deutscher Evangelischer Kirchentag 2017 in Berlin | Christian Mihr
Picha: DW/A. Küppers

Mhariri wa gazeti la Märkische Oderzeitung kuhusu ziara ya Trump barani Ulaya. Mhariri huyo anasema  lingekuwa kosa kubwa kabisaa baada ya ziara hii kumpima siyo kama mwanasiasa, bali kama Trump kwa kaulimbiu ya "Muacheni kwanza, kwa vile bado hajajua vizuri."

Jibu kama hilo linamaanisha kutoa nafasi ya kutaalamika, busara, masikilizano, na utambuzi, kwa kutotumia akili, ujinga na kupenda makuu. Dalili zote zinaonyesha Trump ataendelea kuwepo madarakani kwa miaka minne. Hakuna anaepaswa kutumaini kwamba kunaweza kuwa mchakato wa ufanisi wa kumuondoa madarakani.

Itakuwa miaka minne iliojaa changamoto katika uliwengu unaoendelea kukumbwa na mageuzi ya ghafla na mashaka, kwa sababu Trump anao uwezo wa kuvuruga zaidi utulivu wa dunia. Jumuiya ya kimataifa haipaswi kulichukulia hili kama utaratibu mpya.

Kuhusu muelekeo mpya wa mazingio wa Marekani

Mhariri wa gazeti la Rhein-Neckar ameandika juu ya mkutano wa mataifa saba yalioendelea kiviwanda uliofanyika mjini Sicily Italia. Anasema sasa Ulaya, Canada na Japan zinapaswa kuamua juu ya namna zitakavyoitikia muelekeo mpya wa mazingio wa Markani.

Kwa kufanya hivyo itaonyesha dhahiri kwamba maadili ya jamii ya kimagharibi yanaendelea kulindwa. Jumuiya hiyo imekuwa maskini kwa kupungukiwa na mwanachama mmoja, ingawa ni mmoja wa wanachama muhimu kabisaa.

Wamarekani wakikataa kuchukua uongozi, Ulaya laazima ibebe mustakabali wake mikononi mwake - kama alivyowarai kwa usahihi kabisaa Angela Merkel. Hili halitakuwa rahisi, kwa sababu mataifa ya Ulaya hayako pamoja katika upinzani dhidi ya Trump, kama ilivyoshuhudiwa mjini Sicily.

Rais Donald Trump na mkwe wake Jared Kushner wakiwa katika mkutano na waziri mkuu wa Italia Paolo Gentilioni mjini Rome, Mei 24,2017.Picha: Getty Images/AFP/M. Ngan

kuhusu siku ya Kanisa la Kiprotestant Ujerumani

Mhariri wa gazeti la Ludwigsburger Kreiszeitung ameandika juu ya siku ya Kanisa ilioadhmisha miaka 500 ya kuasisiwa kwa kanisa la Kiprotestant nchini Ujerumani, katika sherehe ambazo zilihudhuriwa na rais mstaafu wa Marekani Barack Obama, zikiwa na kaulimbiu ya kujadili demokrasia.

Mhariri huyo anasema: Siku hii ya Kanisa ilitaka kuwa mfano wa demokrasia ilio hai na hii inajumuisha majadiliano na watu wenye maoni tofauti -  jaribio la kujenga maelewano. Siku ya Kanisa Katoliki mjini Leipzig mwaka 2016 pia iliadhimishwa kwa moyo huo. Nguvu ya kiroho iliotawala mikutano ya madhehebu hayo makuu mawili katika muda uliopita imetoa njia mpya ya kuzungumzia siasa.

Mtu anaweza kuhisi kwamba Ukristo umekuwa nchini Ujerumani. Na hayuko peke yake. Ongezeko la ushiriki wa uchaguzi katika chaguzi zilizopita za majimbo limeonyesha pia kwamba raia wanaanza kutambua kuwa nyakati za mgawanyiko zinahitaji kujishughulisha. Yeyote asiepaza sauti yake sasa, na kushiriki uchaguzi mkuu wa bunge, anawaachia wengine.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/deutsche zeitungen

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW