MigogoroUlaya
Ulaya kuzindua mkakati mpya wa kuachana na nishati ya Urusi
17 Septemba 2025
Matangazo
Kiongozi huyo amesema amechukua hatua hiyo baada ya mazungumzo ya simu na Rais Donald Trump wa Marekani ambaye siku za hivi karibuni ameyarai mataifa ya Ulaya kupunguza au kusitisha kabisa uagizaji mafuta na gesi kutoka Urusi.
Bibi Von der Leyen amesema uchumi wa Urusi unaoendeshwa kwa kutegemea mapato ya nishati za visukuku ndiyo umeiwezesha Moscow kuendelea na vita nchini Ukraine.
Amearifu kwamba Umoja wa Ulaya sasa utatekeleza mkakati utakaorahisisha kuachana na ununuaji mafuta na gesi kutoka Urusi kabla ya mwaka 2028.
Vilevile Umoja huo utatangaza vikwazo ziada vya kiuchumi vitakavyozilenga sekta ya benki na nishati za Urusi.