SiasaAngola
Ulaya na Afrika wakubaliana kushirikiana zaidi
26 Novemba 2025
Matangazo
Tamko la pamoja lilieleza umuhimu wa kuendeleza zaidi ushirikiano na kufungua fursa mpya kwenye maeneo ya kiuchumi, biashara na uwekezaji.
Taarifa hiyo aidha ilirejelea ahadi za awali za ufadhili kwenye mabadiliko ya hali ya hewa na uimarishwaji wa nishati mbadala barani Afrika, lakini pia umuhimu wa kutatua migogoro kote ulimwenguni.
Pande zote mbili zilithibitisha tena kuzingatia demokrasia, utawala bora, utawala wa sheria, haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari.