1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Ulaya na Brazil kukamilisha makubaliano ya biashara

13 Juni 2023

Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema Umoja huo unataraji kukamilisha kufikia mwishoni mwa mwaka huu makubaliano ya kibiashara.

Rais wa Brazil Lula Inacio da Silva akipeana mkono na rais wa Halmashauri kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen alipzuu taifa hilo, Juni 12, 2023.
Makubaliano ya kibiashara kati ya Ulaya na Brazil yalichelewwshwa kwa muda mrefu na hatimaye sasa yatahitimishwa.Picha: Fabio Rodrigues-Pozzebom/Agência Brasil

Von der Leyen aliyeko ziarani katika kanda ya Amerika Kusini,jana huko Brazil alikutana na rais Luiz Inacio Lula da Silva ambaye alikosoa kipengele kilichoongezwa na Umoja wa Ulaya katika mkataba huo,kutokana na wasiwasi wao juu ya kuharibiwa kwa msitu wa Amazon. Mkataba huo umekwama tangu mwaka 2019 kutoka wasiwasi huo wa Umoja wa Ulaya.

Nchi zinazohusika kwenye mkataba huo na Umoja wa Ulaya ni Brazil, Argentina, Paraguay na Uruguay.

Pamoja na kutangaza msaada wa euro bilioni 2 kwa Brazil kwa ajili ya kusimamia uzalishaji wa nishati ya Hydrogen isiyochafua mazingira, Von der Leyen amesifu uongozi wa rais Lula kuhusu sera yake ya mazingira na mpango wake wa kusitisha hatua ya kukatwa miti katika msitu wa Amazon kufikia mwaka 2030.