Ulaya wazungumzia kuipatia Ukraine msaada zaidi wa kijeshi
20 Julai 2023Haya yanajiri huku kukiwa na msukumo wa kimataifa wa kutoa hakikisho la muda mrefu la usalama kwa Ukraine, kama ilivyoamuliwa na viongozi wa kundi la mataifa tajiri duniani G7 pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami NATO wa wiki iliyopita mjini Vilnius huko Lithuania.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa mambo ya Nje wa Ujeruman Annalena Baerbock amesema:
Alisema "Dhamana hizi za usalama zitafanikiwa ikiwa zitakwenda sambamba na hatua tunazochukua katika ngazi ya Ulaya, Jumuiya ya NATO, na katika kundi la G7. Msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine ili kuipa uwezo na haki ya kujilinda, unahitaji fedha za kutosha."
Urusi imeendeleza mashambulizi katika miji ya bandari ya Odessa na Mykolaiv na kuharibu nafaka na miundombinu ya Ukraine.