Ulaya yaibwaga Marekani katika Kombe la Ryder
30 Septemba 2014Matangazo
Ushindi wa timu ya bara la Ulaya dhidi ya Marekani mjini Gleneagles ulikuwa wa kuumiza sana , hususan baada ya matamshi ya Phil Mickelson mchezaji wa timu ya Marekani mwenye uzoefu mkubwa zaidi dhidi ya mchezaji mwenzake Tom Watson.
Ikilinganishwa na wachezaji wa timu ya Ulaya ambayo ina wachezaji kutoka Uingereza, Wales , Scotland , Ireland ya kaskazini, Uhispania, Ufaransa, Ujerumani , Sweden, Denmark na Ufaransa walikuwa na lengo moja tu la ushindi na kuwa pamoja wakiunganishwa na nahodha wao , Paul McGinley.
Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / dpae / rtre , ZR
Mhariri: Iddi Ssessanga