1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yaipa Uturuki bilioni 1 kuwasaidia wakimbizi wa Syria

17 Desemba 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, ametangaza kuwa Uturuki itapokea nyongeza ya msaada wa Euro bilioni moja katika mwaka huu ili kulishughulikia wimbi la wakimbizi wa Syria nchini humo.

Türkei | syrische Geflüchtete in Gaziantep - Erdbeben 2023
Watoto wakitembea katika kambi ya wakimbizi wa Syria nchini Uturuki iliyoanzishwa na shirika la misaada la Uturuki AFAD katika wilaya ya Islahiye ya Gaziantep Februari 15, 2023.Picha: OZAN KOSE/AFP

Von der Leyen amesema ufadhili huo mpya unaongeza kiwango cha fedha cha bilioni 10 ambacho Uturuki imepokea tangu mwaka 2011, kuwasaidia watu waliokuwa wakikimbia mateso ya utawala wa Bashar al-Assad, ambao sasa umeangushwa. Fedha hizo pia zitasaidia katika masuala ya elimu na huduma za afya kwa wakimbizi hao: Uturuki na mataifa ya Umoja wa Ulaya yametoa hifadhi kwa wakimbizi wa Syria, lakini Ankara inasemekana kuwa na idadi kubwa zaidi ya wakimbizi hao nchini mwake wakifikia milioni 3 huku zaidi ya milioni moja wakipewa ulinzi wa kimataifa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW