Ulaya yakumbwa na mafuriko na joto kali
22 Julai 2007Matangazo
Uingereza nayo imeshuhudia mafuriko mabaya kabisa kwa mara ya pili,katika kipindi cha mwezi mmoja. Mamia ya watu katika wilaya ya Worcestershire, walilazimika kuondoka makwao.
Helikopta za kijeshi zimewaokoa zaidi ya watu 100 walionasa kwenye mafuriko,tangu mvua kubwa kuanza kunyesha siku ya Ijumaa.Waziri Mkuu wa Uingereza,Gordon Brown ameahidi kupeleka misaada zaidi katika maeneo yaliyoathirika.
Kwa upande mwingine,idadi ya watu waliokufa kutokana na wimbi la joto kali nchini Rumania,Austria na Bulgaria imefikia 18.Joto kali la juma moja,limeathiri nchi,kuanzia Hungary hadi Ugiriki inayoshuhudia msimu wa joto kali kabisa,tangu zaidi ya karne moja.