1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ulaya yataka Marekani kufikiria upya msaada wake kwa Ukraine

2 Oktoba 2023

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, ametoa wito kwa bunge la Marekani kutafakari upya uamuzi wao kuondoa usaidizi wa fedha kwa Ukraine.

Ukraine | Josep Borrell in Odessa
Picha: Josep Borrell/X/Aton Chile/IMAGO

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell ametoa wito kwa bunge la Marekani kutafakari upya uamuzi wao wa kuondoa usaidizi wa fedha nchini Ukraine baada ya kuridhiwa muswada wa fedha wa muda mfupi unaolenga kunusuru kufungwa kwa shughuli za serikali ya shirikisho.

Akizungumza jana Jumapili mjini Kyiv baada ya mkutano wake na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Borrell amesema anadhani hatua hiyo, haitakuwa ya kudumu na katika siku zijazo Marekani itaendelea kuisaidia Ukraine.

Sheria hiyo iliyoipitishwa Jumamosi inayolenga kuisaida serikali ya shirikisho ya Marekani kujiendesha hadi Novemba 17, imekiweka kando kifungu chenye kutoa nguvu ya msaada wa ziada kwa Ukraine, hatua ambayo ni kipaumbele kwa Rais Joe Biden.

Hata hivyo maafisa wa Ukraine wamesisitiza kwamba uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine ungepaswa kuendelea licha ya sheria hiyo.