Ulaya yaziwekea vikwazo kampuni zinazochangia vita Sudan
22 Januari 2024Matangazo
Baraza hilo limesema kwenye taarifa kwamba kampuni hizo sita zilikuwa zikihusika na kuunga mkono shughuli zilizodhoofisha utulivu na mabadiliko ya kisiasa nchini Sudan.
Kampuni mbili kwenye orodha hiyo zinajihusisha na uzalishaji wa silaha na magari ya kijeshi kwa ajili ya jeshi la Sudan, SAF, na matatu zinazofanya manunuzi ya vifaa vya kijeshi kwa ajili ya RSF.
Baraza hilo limesema mali za kampuni hizo zitazuiwa na hazitaruhusiwa kutoa ufadhili kwa ajili yao ama kwa ajili ya maslahi yao.