1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulimwengu kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili

Florence Majani23 Novemba 2021

Wakati dunia ikielekea katika maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Tanzania zinaeleza kuwa watoto 6,168 walifanyiwa ukatili wa kijinsia, 3,524 walibakwa.

Ägypten Protest gegen sexuelle Belästigung
Picha: picture-alliance/AP Photo/A. Nabil

Wakati ripoti hiyo ikionyesha hayo, huko wilayani Kibondo, mkoani Kigoma Naibu Waziri wa Afya, Mwanaidi Ali Khamisi alikutana na takwimu zinazofanana na hizo, zikionyesha kuwa wanafuzi 980 walipata mimba katika kipindi cha Januari hadi Juni 2021. Hayo yote yanajiri wakati dunia inaadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Akizungumzia hali ya ubakaji nchini na maadhimisho ya mwaka huu, Mkuu wa Mawasiliano serikalini kutoka Wizara ya Afya, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Prudence Constantine amesema, serikali inajitahidi kupambana na kupunguza au kumaliza kabisa ukatili wa kijinsia na hivyo akataka kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki vita hivyo.

Prudence ameshauri kuwa katika kipindi hiki cha Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia,  jamii lazima ioneshe kuwa inakerwa na haifurahisshwi na vitendo hivi.

mwananmke akishiriki maandamano y akupinga ukatiliPicha: Getty Images/AFP/A. Shazily

Madawati ya jinsia yaliyopo kwenye jeshi la polisi hutumika katika kutatua migogoro ya unyanyasaji wa kijinsia, likiwamo hili la ubakaji.  SSP Leah Mabunda ni Mkuu wa Dawati la Jinsia kanda ya  Maalum ya Dar es Salaam:

Mkurugenzi wa Asasi ya Viongozi Wanawake Vijana(YWLP) na Mwanaharakati wa masuala ya jisnia, Consolat Chikoti, amesema jamii inapaswa kujua wajibu wake katika kumaliza tatizo la ubakaji nchini.

Kwa upande wake, mkaazi huyu wa Jijini Dar es  Salaam, mwenyewe akiwa mama wa watoto wawili, Sauda Msangi, anatoa angalizo kwa wazazi na walezi kuwa makini katika kuwaangalia watoto ikiwamo kuondoa tabia hatarishi zinazochochea mazingira ya ubakaji.

Katika ripoti hiyo iliyotolewa na Naibu Waziri wa Afya akiwa bungeni, maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka huu yanapambwa na kauli mbiu isemayo: Komesha ukatili wa kijinsia sasa.