1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulimwengu unaomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II

9 Septemba 2022

Baada ya zaidi ya miaka 70 kwenye kiti cha ufalme, akitawala kwa muda mrefu zaidi nchini Uingereza amefariki akiwa na umri wa miaka 96. Aliaga dunia katika Kasri la Balmoral huko Scotland.

Queen Elizabeth II
Picha: Frank Augstein/WPA Pool/Getty Images

Mataifa mbalimbali yameendelea kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza, salamu za hivi karibu ni kutoka kwa Mfalme Felipe wa Uhispania, amabe kupitia ukurasa wake wa telegramu ameipa pole familia ya kifalme. Kiongozi huyo ameeleza wanafamilia wote wapo katika mioyo yao na kwamba watamkumbuka malkia daima.

Rais wa Marekani Joe Biden naev ametoa salamu zake rambirambi kwa malikia hiyo ambae katika siku za uwahi wake amewahi kukutana na marais wa Marekani 14, akikukumbuka mkutano wake wa mwisho ambao akielezea ukarimu wake, upendo na busara zake.

Aidha Biden alimweleza kuwa katika ulimwengu wa mabadiliko ya mara kwa mara, akiwa mshiriki thabiti na chanzo cha faraja na fahari kwa vizazi vya Uingereza.

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amesema Malkia Elizabeth II ni alama ya ulimwengu.

Malkia Elizabeth II wakati wa uhai wakePicha: Orban Thierry/abaca/picture alliance

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amesema Malkia Elizabeth II alikuwa mfano wa kuigwa na mtoa hamasa kwa mamilioni ya watu wakiwemo Wajerumani.

Scholz alisema kujitoa kwake katika kufanikisha maridhiano ya Ujerumani na Uingereza baada ya mambo mabaya ya Vita Vikuu vya Kidunia hakuijasahaulika.

Amesema hatosahaulika sio tu kwa ukaribu wake wa kiwango cha juu bali kwa mengi. Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema Malkia Elizabeth alkiuwa wakati wote katika maisha ya watu na huduma yake kwa Watu wa Canada itasaliwa kuwa sehemu muhimu daima katika historia ya taifa lao.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika ukurasa wake wa Twitter amemulezea kama mtu mwenye kujali utu na kuheshimu maisha ya watu, na kuonesha kusikitishwa sana na kifo hicho.

Pole ya Rais Rais Vladimir Putin kwa watu wa Uingereza.

Katika ujumbe wake kwa Mfalme mpya wa Uingereza, Charles, Rais Vladimir Putin wa Urusi ametoa pole kwa watu wa Uingereza na kuwataka kuwa wenye ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu.

Wengine waliotoa salamu kama hizo ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Anthonio Guterres, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na Rais wa Ghana Nana Akufo-Ado.

Kifo cha Malkia Elizabeth II

Malkia Elizabeth ambae amefariki dunia jana Alhamis anatajwa kama kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini humo na kuipitisha Uingereza katika nyakazi ngumu na nyepesi katika kipindi chote cha utawala wake wa miaka 70. Kfo chake kimetokea akiwa na umri wa miaka 96.

Kasi ya Buckingham imetangaza kwamba Malkia amefariki akiwa katika kasri ya Balmoral huko Scotland ambako huwa anapumzika katika majira ya joto.

Soma zaidi:Malkia Elizabeth II afariki dunia

Mwanae Prince Charles mwenye miaka 73 ndio anakuwa mfalme, ingawa kuthibitishwa kwake kunaweza kuchukua miezi kadhaa. Haijulikani iwapo atajiita mfalme Charles III ama atajiita majina mengine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW