JamiiMarekani
Guterres aunda jopo kuangazia matumizi ya Akili ya kubuni
27 Oktoba 2023Matangazo
Guterres amesema licha ya teknolojia hii ya Akili ya kubuni kuwa muhimu lakini inatishia demokrasia na haki za binaadamu.
Guterres amelitaka jopo hilo kuharakisha mchakato wa kuandaa mapendekezo yatakayoainisha namna ya kudhibiti matumizi ya AI hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2023, kuanzia kitisho hadi fursa zinazokuja na teknolojia hiyo.
Guterres amechagua jopo la wataalamu 40 wa teknolojia na ulinzi wa taarifa binafsi, wakati akiashiria mashaka yanayoibuliwa na teknolojia hiyo ambayo ni pamoja na upotoshwaji wa taarifa, ubaguzi, ufuatiliaji na uingiliaji wa faragha.