Wakati hivi leo ulimwengu ukiadhimisha siku ya Sayari ya Dunia, Jimi Cohen, raia wa Australia na mwanzilishi mwenza wa shirika la Treegens DAO, ameweka rekodi ya kupanda miti mingi zaidi kwa kipindi cha masaa 24.
Matangazo
Cohen amefanikiwa kuipanda mikoko elfu 30,279 katika eneo la Majoreni, Kaunti ya Kwale, iliyoko Pwani ya Kenya akivunja rekodi iliyokuwa imewekwa na Antoinne Moses, raia wa Canada aliyepanda miti elfu 23,060 mwaka 2021.
Tangu jana, mwendo wa saa sita mchana, raia huyu wa Australia alianza upandaji wa miche ya mikoko katika eneo la Majoreni, Kaunti ya Kwale, hapa Pwani ya Kenya. Shughuli hiyo imekamilika leo Jumatatu, wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya Sayari ya Dunia.
Cohen anasema azma hii imechangiwa na jitihada za kutumia miti kusafisha mazingira na kuishawishi dunia kuchukua hatua ya kuyalinda mazingira. Kulingana naye, alilichagua bara la Afrika na hasa Pwani ya Kenya kwa sababu ya usalama na pia kuvutiwa na watu wa Majoreni, ambao wamekuwa wakipanda mikoko kuyalinda mazingira. “Ni nchi ya kuvutia na ina mandari ya kupendeza na wenyeji pia wanayajali mazingira na ni kuzuri kwa kupanda mikoko, nchini australia kupanda mikoko kuna changamoto kwa sababu kuna mamba wengi kwa hiyo si salama ndio maana nilichagua Kenya, hata watu wanaelewa kuhusu mazingira. Hii ni Mara yangu ya tatu kujaribu kuvunja rekodi, ikotokea sijafaulu basi haitakuwa mwisho wangu nitajaribu Tena.”
Hii ni mara yake ya tatu kujaribu kuvunja rekodi hii ya upandaji wa miche. Anasema amekuwa akifanya mazoezi kwa takribani mwaka mmoja. Kabla ya kutunukiwa taji hilo, shughuli nzima itaratibiwa na shirika la Guiness World Record. Iwapo atashinda, Cohen atakuwa binadamu wa kwanza duniani kupanda miche zaidi ya elfu thelathini ya mikoko kwa masaa 24 mfululizo.
Livingstone Kitawi, afisa wa Idara ya kuhifadhi misitu nchini Kenya pamoja na wenzake waliongoza shughuli ya kunakili idadi ya miche pamoja na kumlinda. “tumeweza kusaidia katika kuhesabu, kipindi cha kwanza tulikuwa tunafanya masaa manne manne,halafu napumzika napisha wenzangu, tulikuwa zaidi ya watu nane hapo tukibadilishana kwa hayo masaa ishirini na nne,tumeweza kutembea na wao na pia tukajua uwezo wetu kuwa tunaweza kufanya kazi masaa ishirini na nne bila kupumzika na pia bila kuchoka .“
Bahari: Msaada wa Maisha ya Dunia
Bahari inachukuwa sehemu kubwa ya sayari ya dunia na inasaidia kuratibu mabadiliko ya tabianchi - lakini sehemu yake kubwa bado ni mafumbo kwa wanasayansi
Picha: Getty Images/M. Tama
Sayari yetu ya buluu
Sio kwamba inaitwa sayari ya buluu bila ya sababu. Bahari imechukuwa 71% ya uso wa dunia na 90% ya pembe zake. Inategemewa sana na maisha na inatoa baina ya 50% na 80% ya hewa ya oksijini, kunakoifanya kuwa sehemu muhimu sana ya mzunguko wa hewa ya ukaa. Asili ya bahari bado haifahamiki, lakini inafikiriwa kuwa iliundika miaka bilioni 4.4 iliyopita na kuwa kiini cha awali cha uhai.
Picha: NASA
Jinsi maisha yalivyo
Hivi sasa wanaishi takribani viumbe wa aina 230,000 baharini. Matumbawe chini ya bahari ni maficho kwa samaki kama kaa, pweza na kamba na wengine wenye rangi za kupendeza. Mimea humea huko chini huku viumbe wakubwa kama papa, nyangumi na pomboo wakipita kwenye vina vya wazi vya maji.
Picha: picture-alliance/blickwinkel
Mafumbo chini ya kina cha maji
Licha ya ukubwa wake, tunajuwa machache sana kuhusu dunia. Kwa hakika, zaidi 80% ya maisha ya chini ya bahari hayajafikiwa. Wanasayansi wanajaribu kuyafumbuwa mafumbo yake, ambako kutatusaidia kuyafahamu vyema zaidi mabadiliko ya mazingira na jinsi ya kuzisimamia vyema rasilimali za bahari.
Picha: Colourbox/S. Dmytro
Viumbe vya ajabu na vinavyotisha
Wanasayansi wanaamini pia kwamba zaidi ya nusu ya aina wa viumbe vya bahari hawajagundulika. Lakini watafiti wanazipata aina mpya kila mwaka - wengi wao wakiwa ni tafauti kabisa na waliowahi kufahamika kabla, kama huyu nyungwi bahari (pichani) aliyegunduliwa kwenye Bahari ya Celebes mwaka 2007. Kile kilichobakia huko chini hakuna ajuwaye.
Picha: Laurence Madin, WHOI
Mratibu wa mabadiliko ya tabianchi
Bahari ina jukumu sana kwenye kuratibu tabianchi ya sayari ya dunia kwa kufyonza mionzi ya jua, kuchawanya joto na kuendesha mwenendo wa hali ya hewa. Lakini mabadiliko ya tabianchi tayari yameanza kuharibu uwiano huu, yakiathiri uwezo wa bahari kutelekeza majukumu yake ya kimsingi kwenye mfumo wa kimaumbile, kama vile uhifadhi wa ukaa na utoaji wa oksijini.
Dalili za indhari
Moja ya dalili za mabadiliko ya tabianchi ni ongezeko la kuchujuka kwa matumbawe. Kuongezeka kwa joto na uharibifu wa mazingira unayachafua matumbawe na kusababisha yatowe aina maalum ya algae ambayo inayawezesha kukuwa na kuzalisha na nyuma yake ikawacha mifupa ya kutisha. Matumbawe mengine yanaweza kurejea upya, lakini vitu vinavyoyaharibu vikiendelea kwa muda mrefu huongeza vifo vya matumbawe.
Picha: XL Catlin Seaview Survey
Hapana pa kukimbilia
Mabadiliko ya tabianchi yanaathiri pia maisha ya viumbe vya baharini, huku utafiti wa karibuni ukionesha samaki, pweza na kaa wakitoweka mara mbili zaidi ya viumbe vya ardhini. Joto kali ni chanzo kiku kwani bahari zina maeneo machache ya kujificha. Kwa masikitiko, viumbe vya bahari havitaweza kujibadilisha haraka vya kutosha kuweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Eneo lililoganda barafu
Kupanda kwa joto duniani kunapelekea kuyeyuka kwa mapande ya barafu katika eneo la dunia lililoganda theluji.
Picha: DW/Irene Quaile
Myeyuko mkubwa?
Barafu inayeyuka
Picha: Getty Images/M. Tama
Picha 91 | 9
Wanakijiji wa Majoreni wameiambia kuwa wafurahishwa kwa kijiji chao kuchaguliwa kwa kampeni hii. Mmoja wao, Omari Bakari, anasema miche iliyopandwa imewapunguzia kazi kubwa wanamazingira. Bakari ameahidi kufuatilia miche hiyo kuhakikisha imechipua. siku ya Leo tukona furaha, mwanzo sisi ndio huwa walindaji bora wa mazingira, kuna Kama vikundi vinne vya wapanzi wa miti katika sehemu yetu Hii ya majoreni.”
Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu wa 2024 kwa Siku ya Sayari ulimwenguni ni "Sayari Dhidi ya Plastiki", ikitowa ujumbe wa kuongeza ufahamu wa watu kuhusu hatari za kiafya za plastiki, kwa lengo la kukomesha matumizi ya plastiki. Siku hii ilianza kuadhimishwa mwaka 1970 nchini Marekani.