Ulimwengu waukaribisha mwaka mpya kwa onyesho la fashifashi
1 Januari 2025Matangazo
Mataifa ya mwisho mwisho kushuhudia mwaka mpya ni pamoja na Brazil ambako karibu watu milioni 2.5 walihuhudhuria onesho la fashifashi kwenye fukwe maarufu za Copacabana mjini Rio de Janeiro.
Soma pia: Heri ya mwaka mpya! Ulimwengu wakaribisha 2025
Mamia kwa maelfu walikusanyika pia kwenye uwanja wa Times Square mjini New York, Marekani kushuhudia kuanza kwa mwaka 2025 wiki kadhaa kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Donald Trump kuliongoza tena taifa hilo kwa muhula wa pili wa miaka minne.
Hapa Ujerumani mbali ya miji mingine, maelfu walikusanyika pia mbele ya Lango mashuhuri la Brandenburg mjini Berlin, kwa onesho la fataki.