1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

UM: Urusi imezidisha mashambulizi ya droni Ukraine

15 Novemba 2024

Umoja wa Mataifa umesema jeshi la Urusi limezidisha mashambulizi ya droni na kuwalenga raia pamoja na miundombinu ya nishati ya Ukraine ambayo imeharibiwa kwa asilimia 65.

Athari ya mashambulizi ya droni za Urusi nchini Ukraine
Athari ya mashambulizi ya droni za Urusi nchini Ukraine.Picha: Serhii Chuzavkov/Avalon/Photoshot/picture alliance

Matthias Schmale, mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, ametahadharisha hivi leo juu ya uwezekano wa mashambulizi hayo kusababisha ongezeko la idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani.

Schmale amesema watu milioni 3.6 tayari ni wakimbizi wa ndani nchini Ukraine na baadhi yao wamekuwa wakiishi katika makazi ya dharura kwa miaka miwili au zaidi. Mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa mashambulizi hayo ya droni hutumiwa "ugaidi wa kisaikolojia."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW