1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umati wa mahujaji umewasili mjini Makkah

24 Juni 2023

Mamilioni ya mahujaji wamewasili katika mji mtakatifu wa waislamu, Makkah kwa ajili ya kufanya hija. Hajj ya mwaka huu ni ya kwanza tangu mwaka 2019 ambapo mahujaji wanahudhuria bila ya vikwazo vya corona.

Vorbereitung auf den Haddsch
Picha: Amr Nabil/AP Photo7picture alliance

Maafisa wa Saudi Arabia wamesema karibu watu milioni 1.5 tayari wamewasili nchini humo. Kuhiji ni moja ya nguzo tano za Uislamu na Waislamu wote wenye uwezo wanatakiwa kuitekeleza angalau mara moja katika maisha yao.

Waziri anayesimamia maswala ya Hijja na Umra wa Saudi Arabia, Tawfiq Al-Rabiah, amesema watu milioni 2 kutoka nchi zaidi ya 160 wanatarajiwa kuhimili joto kali wakati wanaposhiriki nguzo hiyo muhimu ya Uislamu. Shughuli za kufanya Hijja zitaanza siku ya Jumatatu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW